Mama ajuta baada ya kumtendea mumewe ukatili Mayor Road,Ongata Rongai

Global Alerts

by Toter 41 Views 0 comments

Felix mwenye umri wa miaka thelathini na mmoja na Bridgit mwenye miaka ishirini na sita ni wanandoa ambao walioana miaka minne iliyopita. Wawili hao walijaaliwa kumpata mtoto mmoja wa kike kabla hawajoana rasmi. Juma lililopita, mambo yalichacha na kuchemka baada ya Felix kujitokeza waziwazi kwa kuyaweka paruwanza mambo yaliyomsibu. “Tukiwa tunachumbiana nilimpachika mimba Bridgit mimba hali iliyonilazimu kumuoa baada ya shinikizo kutoka kwa wazazi wake,”Felix alifichua. Ufichuzi huu uliwaacha wakaazi wa Mayor katika hali ya mshangao Kwa kile alichodai kuwa hakuwa na hisia za mapenzi kwa Bridgit. Screenshot “Sikumpenda kamwe,” Felix alisisitiza. Masaibu ya Felix yalianza tu pindi mwanawe alipofika mwaka mmoja unusu; mke huyu katili mwenye kiburi chungu nzima alianza kumdharau mume wake. Hakumtambua Felix kama mumewe, aliyaasi majukumu yake kama mkewe, kwa mfano alifeli kumpikia chakula mumewe, kumfulia nguo, kutumwa na mumewe na mengine mengi. Hata tendo la ndoa alikuwa akimnyima mumewe bila sababu za msingi. Hali hii ilizidi kuzorota zaidi na zaidi mwaka jana, baada ya Bridgit kuandamana na mwanawe mchanga hadi Felix alikokua akifanya kazi yake ya useremala na kumtundika mtoto kwenye sakafu ya jengo hilo na kuapa ya kwamba hayuko tayari kuwa mkewe Felix. Ilimlazimu Felix kufunga kazi yake ili amshughulikie mtoto kwa sababu mtoto...

0 Comments